Burudani ya Michezo Live

UFC 207: Amanda Nunes amchakaza Ronda Rousey ndani ya sekunde 48!

Ronda Rousey hakuweza kuhimili makonde mazito toka kwa Mbrazil, Amanda Nunes aliyemchakaza kwenye pambano la UFC 207 la ubingwa wa bantamweight, lililofanyika Las Vegas, asubuhi ya Jumamosi kwa saa za Afrika Mashariki.

https://youtu.be/wMXVBj3L5as

Pambano lilianza kwa Nunes kurusha makonde mfululizo kwa Rousey yaliyomwelemea na kuchakazwa ndani ya sekunde 48 tu za pambano hilo na kumfanya mwamuzi, Herb Dean asitishe pambano.

Rousey hakuamini kama angeweza kudundwa katika muda huo mfupi na kuna wakati alitaka kuanguka wakati amesimama kutafakari kilichotokea ndani ya sekunde chache tu.

Hilo linakuwa pigo jingine kubwa katika career ya bondia huyo ambaye mwaka uliopita alipoteza tena pambano jingine dhidi ya Holly Holm kwa fedheha kubwa.

Swali ambalo watu wengi wanajiuliza sasa ni iwapo Ronda ataendelea tena ngumi ama ataamua kustaafu kabisa.

SHARE THIS

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW