Bongo Movie

Usitegemee stori mpya za filamu, tunaboresha zilizopita – Gabo

Msanii wa filamu, Gabo Zigamba amewataka watanzania kujua kwamba hakuna stori mpya ambayo wataifanya wasanii wa filamu, kwani stori nyingi zimeshatumika ila wanachokifanya kwa sasa ni kuboresha stori na kuiingiza kwenye uhalisia wa watanzania.

Akiongea na Bongo5 Jumatano hii wakati akizindua filamu yake mpya ya Kisogo, Gabo alidai hakuna kitu kipya ambacho kitafanywa na wasanii wa filamu kikaonekana ni cha kwanza kuonekana au kufanyika duniani.

“Unajua watu wanashindwa kuelewa kwenye ishu za stori zetu za filamu, wanasema stori ni zile zile na wanataka stori mpya wanashindwa kutambua hakuna stori ambayo utaitoa ukasema hii haijawahi kutumika duniani,” alisema Gabo. “Kila stori ambayo unaiona kwenye filamu ni stori ambayo tayari iliwahi kutumika sehemu fulani sisi tunachokifanya ni kuboresha wazo na kupata kitu kipya,”

Muigizaji huyo alisema ameamua kulivalia njuga suala la kuikomboa tasnia ya filamu na kuhakikisha watu wanarudisha imani kwa filamu za ndani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents