Afya

Utafiti: Chuki kwa bosi na kutosafisha meno ni miongoni mwa sababu za kupata kiharusi

Sote tunafahamu kwamba tumbaku ,unene wa mwili kupita kiasi na ukosefu wa mazoezi vinaweza kuongeza uwezekano wako wa kupata kiharusi.

lakini kuna mambo mengine ambayo huenda hujawahi kuyasikia yanayoweza kusababisha maradhi hayo.

Maradhi ya moyo yanaongoza kwa kusababisha vifo kwa mujibu wa data zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Fahamu mambo 5 yanayoweza kusababisha kiharusi kwa mujibu wa tafiti mbalimbali DUNIANI.

1. Kutosafisha meno

Uchunguzi kadhaa umeonyesha kuwa wenye afya mbaya ya kinywa wana uwezekano mkubwa wa kupata matatizo ya moyo.

Fizi zenye majeraha huwawezesha bakteria kuingia kwenye mfumo mzima wa damu.

Zinaweza kusaidia kukwama kwa mafuta kwenye mishipa ya damu.

2. Chuki dhidi ya bosi wako

Si jambo la mzaha – kumchukia bosi wako kunaweza kukusababishia matatizo ya afya ya moyo.

Utafiti uliofanywa kwa miaka 10 nchini Uswisi na kuchapishwa kwneye jarida la tiba la Uingereza- British Medical Journal ulibaini kwamba uhusiano mbaya na kiongozi wako kazini huongeza uwezekano wa shinikizo la damu kwa asilimia 40% ya watu.

3. Tukio linaloshitua

Taarifa ya ghafla inayokushitua mfano kifo cha mtu wa familia yako inaweza kukusababishia kiharusi.

Kwa mujibu wa shirika la afya ya wanawake waliotimiza umri wa kutoweza kupata ujauzito nchini Marekani , mishipa ya damu miongoni mwa wanawake ambao wamewahikupitia matukio matatu ya kushitua maishani mwao, uwezo wao wa kufanya kazi ni mbaya wakilinganishwa na wanawake ambao hawajawahi kupitia uzoefu huo.

4. Kujihisi mpweke

Jarida jingine la kitabibu la Uingereza linaonyesha kuwa watu wenye mahusiano ya kijamii na watu wachache wanakabiliwa na uwezekano wa asilimia zaidi ya 29% ya kupatwa na maradhi ya moyona asilimia 32% zaidi ya uwezekano wa kupata kiharusi.

5. Msongo wa mawazo

Shirika linalojishughulisha na masuala ya afya ya moyo linasema kuwa 33% ya wagonjwa wa shinikizo la damu nchini Marekani hupata ugonjwa huo kutokana na msongo wa mawazo.

Wataalamu wanashuku kwamba watu wenye matatizo ya afya ya akiliwanaweza kuhisi ugumu wa kuchukua maamuzi ya kiafya.

Source: BBC


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents