Diamond PlatnumzVideos

Video: Chege abaraki uamuzi wa Diamond kurekodi wimbo kwa beat ya Uswazi Take Away

Chege Chigunda anakichukulia kitendo cha Diamond Platnumz kurekodi wimbo kwa kutumia beat ya ngoma yake Uswazi Take Away kama heshima kubwa kwake.

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni kwenye uzinduzi wa video mpya ya Diamond Platnumz, Number 1, Chege amesema uamuzi huo umemfurahisha pia meneja wake.

“Unajua watu hawakuwahi kutegemea kwamba Diamond anaweza akafanya hivyo, kwamba ngoma kafanya Chege ‘naomba beat nifanye mimi’. Kwa mimi sikuona sababu ya kuwa na makubaliano makubwa ingawa mimi naijua haki yangu ni nini natakiwa kupata nini kwa yeye kufanya vile lakini naamimi na yeye pia anajua uthamani wa kile kitu, kwanini alikuja kuniomba? Anajua thamani yangu na mimi kwanini nilikubali, najua thamani yake. So kitu kiko fair yeye kufanya na ni kitu kikali nimefurahi kwasababu amekifanya kitu nilichokifanya mimi, mimi nilifanya ngoma kali na yeye amefanya ngoma kali sana,” alisema Chege.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents