Habari

Video: Ni kweli tuliahidi milioni 50 kwa kila kijiji – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa ni kweli waliahidi milioni 50, 50 kwa kila kijiji lakini ameona ni vyema aanze na mambo ya jumla ya Watanzania huku akieleza kuwa hiyo ahadi itakuja tu.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana jioni wakati akihutubia mkutano wa hadhara mjini Mwanza ambapo amesema kuwa ukitengeneza reli ya kutoka Dar es salaam mpaka Mwanza kufika tu Dodoma zimechukuliwa Trilioni 7 wangezigawa hizo Trilioni kwa vijiji vyote wangekuwa washamaliza.

“Kupanga ni kuchagua ndio maana wengine walikuwa wananiambia uliahidi milioni 50, 50 kwa kila kijiji ni kweli tuliahidi lakini nilipoingia huku nilikuta mambo yako mengi ambayo yanaweza yakazaa hiyo milioni 50, 50, ukitengeneza treni, reli ya kutoka Dar es salaam mpaka Mwanza kutoka tu Dodoma zimechukuliwa Trilioni 7 tungezigawa hizo Trilioni kwa vijiji vyote si tungekuwa tushamaliza,” alisema Rais Magufuli.

“Lakini kupanga ni kuchagua nianze kugawa hizo 50, 50 au nianze treni ambayo itazaa mapema nianze na kugawa 50,50 au nijenge kwanza Seketule watu watibiwe,niache kujenga daraja la Furahisha watoto wawe wanagongwa au niwape 50, 50 kwahiyo niliona nianze na mambo makubwa ya Wtanzania hiyo ahadi itakuja tu.”

Rais Magufuli yupo mjini Mwanza kwa ziara ya siku mbili ya kikazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents