Technology

Video: Wasichana wa Kenya watengeneza App ya kukomesha ukeketaji

Wasichana kutoka katika mji wa Kisumu nchini Kenya wametengeneza programu ya kusaidia kukabiliana na ukeketaji kwa wanawake.

Wakiongea na shirika la habari la BBC, wanafunzi hao wamesema, wameamua kutengeneza App hiyo iitwayo iCut ili kuwasaidia wasichana wanaopitia kwenye janga la ukeketaji huku wengi wao wakiwa hawana elimu ya madhara yake.

“Tuliamua kutengeneza App inayoitwa iCut. Na hii App inasaidia wasichana ambao wanapitia ukeketaji na wengi wao hawaelewi ni nini madhara ya kupitia ukeketaji, lakini wengine wanajua ingawa hawawezi kusaidiwa kutoka kwenye shida hiyo,” wamesema wanafunzi hao.

https://www.facebook.com/BBCSwahili/videos/1643004679051524/

“Tunaelewa kuna madhara mengi sana kama Anemia, mtu anaweza kufa kwa wakati huo na pia kuna madhara mengine kwa wanawake wakati wa kuzaa ndio nikaamua lazima nikomeshe ukeketaji,” wameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents