Siasa

Video ya Obama na Romney wakichuana kwenye rap battle

Zikiwa zimebaki siku chache tu hadi November 6 ambapo uchaguzi wa urais wa Marekani utafanyika, kumekuwepo na mjadala mkali kuhusu nani atashinda kati ya rais anayetetea kiti chake Barack Obama wa chama cha Democratic na Mitt Romney wa Republican. Hata hivyo kwa mujibu wa matokeo ya midahalo yote mitatu iliyofanyika, Obama ameonekana kufanya vizuri zaidi ya mpinzani wake.

Lakini pia watu wamekuwa wabunifu kwa kutengeneza video za utani za wagombea hao kama video hii iliyojichukulia umaarufu kwenye mtandao wa Youtube ambapo ikiwa na wiki moja tu tayari imeangaliwa kwa zaidi ya mara milioni 15. Ikiwa imepewa jina la ‘Barack Obama vs Mitt Romney. Epic Rap Battles Of History Season 2’ inawaonesha watu wawili wenye mfanano na wagombea hao wakiangusha mistari ya utani katika beat moja kali ya Hip Hop.

Tunaamini utaenjoy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents