Habari

Viongozi igeni mfano wa Makonda, msijifungie ofisini, jifichueni wananchi wawaone

Ukiwa una kipaji hakuna mtu anayeweza kukuona ukiwa umejificha nyumbani au umekaa sehemu ukitegemea mtu ahisi wewe una kipaji. Ni vyema mtu kujitokeza ili watu na jamii kwa ujumla wajue ni nini unacho ndani yako zaidi sana wakupe maksi na kukupongeza kwa kufanya jitihada za kujitokeza jamii ikiwa tayari imeshakuona.

14276379_114664568992748_1632110335_n-1

Kwanini ujitokeze?

Mpaka hivi sasa ninavyoandika Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ana ziara ya siku kumi ndani ya jiji lake lengo ni kutatua kero za wananchi wa jiji hilo pamoja na kutatua kero zao zinazowazunguka. Zoezi hili la kuzunguka katika mkoa wake ni kutaka kutengeneza ‘Dar Mpya’ ambayo ni ya tofauti na ile watu waliyoizoea.

Tumegundua nini katika ziara ya Mkuu wa Mkoa huyo?

Kumbe viongozi wakikaa ofisini tu haitoshi,wamepewa dhamana ya uongozi kupitia wananchi na wananchi wamewapa dhamana ya kuwatumikia ili waweze kutambua matatizo na adha wanazokumbana nazo na viongozi wa chini. Ukikaa ofisini kama kiongozi hautaweza kutatua shida za wananchi zinazowapata wananchi wako kwa hiyo ni vyema sana ukitembea maeneo mbalimbali kujua shida za wananchi wako.

Katika ziara ya Makonda tumeona nini?

Tumeona wananchi wakinyanyaswa na viongozi pamoja na kupewa ahadi za uongo zisizojulikana ni lini hatma ya utatuzi wake,sambamba na baadhi ya wajane wakidhulumiwa ardhi, mashamba,huku wengine wakilalamika kupewa adhabu na polisi ambazo ni kinyume na utaratibu uliowekwa.

Utaratibu wa ujibiwaji wa utekelezwaji wa matatizo ulikuwa vipi?

Mkuu wa mkoa huyo alikuwa na timu yake ya viongozi mbalimbali husika kila mtu na kitengo chake akitaka majibu yatolewe mbele ya wananchi huku akiruhusu wananchi kusema kama kiongozi huyo kaongea ukweli au uongo ili Mkuu wa Mkoa huyo ajue ni nini kinaendelea kwa kiongozi sambamba na mkuu wa mkoa huyo kuweka umakini kusikiliza viongozi hao wakijitetea.

Kwanini ni Dar es salaam tu?

Yeye kama mkuu wa mkoa huo ameamua kuzunguka katika jiji lake ili kutambua adha mbalimbali za wananchi wake ili aweze kutengeneza Dar Mpya ambapo kiongozi huyo alishawahi kusema kuwa anatamani siku moja Dar es Salaam ifanane na Dubai mtu ukiacha pochi unaikuta. Lengo ni kutengeneza Dar mpya yenye muonekano mpya.

Tujifunze haya viongozi wengine

Nikurudishe nyuma kidogo Makonda amekuwa ni moja ya viongozi ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kutetea wananchi wake. Alishawahi kujitoa kumsaidia kijana Saidy Ally Mrisho aliyetobolewa macho maeneo ya Buguruni Sheli jijini Dar es Salaam. Alimfuata nyumbani kwake kwa kutaka kujua nini kimemsibu kiongozi huyo. Asingeenda nyumbani kwake huenda asingejua kilichompata kijana huyo aliye katika mkoa wake. Amejitahidi kuonesha jitihada juu ya kusaidia na wengine na Jumanne hii amemsaidia mzee mmoja aliyekuwa katika ziara yake papo hapo na aliimsaidia kiasi cha fedha na kumpa mkuu wa wilaya ili aweze kumkabidhi.

Hata maandiko yanasema baraka za Mungu zipo kwa wale ambao wanalia na wenye shida na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanyonge walio dhulumiwa,walioonewa,walionyanyaswa na wengine wengi lengo ikiwa ni kutengeneza amani kwa kila Mtanzania sambamba na kuondoa matabaka ya walio nacho na wasio kuwa nacho ili kuijenga na kulinda taifa na amani ya nchi yetu – amani ambayo baadhi ya nchi za wenzetu hawana.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents