Promotion

Vodacom yaibuka na ‘Bingo’ ya Tuzo Pointi

Vodacom TuzoKAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom, imezindua ‘Bingo’ ya sh. bilioni moja ikiwa ni programu mpya ya uaminifu ijulikanayo kama Tuzo Pointi

Vodacom Tuzo

 

 

 

Na Grace Michael

 

 

 

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom, imezindua ‘Bingo’ ya sh. bilioni moja ikiwa ni programu mpya ya uaminifu ijulikanayo kama Tuzo Pointi ambayo itakuwa ikitoa zawadi kwa wateja wake, baada ya kujibu maswali ambayo yatawapa pointi ambazo zitakuwa zikizingatiwa katika utoaji wa zawadi hizo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa Matukio na Promosheni wa Vodacom, Bibi Rukia Mtingwa, alisema programu hiyo ni moja ya mikakati ya kampuni hiyo kuboresha huduma kwa wateja wake.

 

Alisema ili kutoa shukrani kwa wateja wa kampuni hiyo, wameona njia sahihi ya kuwafikia nchini kote ni kuandaa programu hiyo ambayo itawasaidia wateja wa kampuni ambao wameiwezesha kufikia mafanikio iliyonayo.

 

“Programu yetu ya Tuzo Pointi ni sehemu ya mkakati wetu endelevu wa kuwazawadia wateja wetu ambao wametuwezesha sisi kuwa mtandao unaoongoza Tanzania,” alisema Bibi Mtingwa.

 

Alisema programu hiyo itamfanya mteja kujinyakulia pointi kwa njia tatu ambapo kila atakapotumia sh. 100 atapata pointi moja, njia nyingine ni kuongea.

 

Alifafanua kuwa mteja akipokea simu na kuongea kwa dakika moja, atajiongezea pointi nyingine.

 

Aliitaja njia ya tatu kuwa ni mteja atakapoendelea kuwa kwenye mtandao wa Vodacom kwa wiki moja, atapata pointi nyingine.

 

Alisema pia sehemu ya pili ya programu hiyo ni Tuzo Droo ambapo mteja atajishindia mamilioni ya fedha kila wiki.

 

Alifafanua kuwa mteja atajishindia sh. milioni 40 kila mwezi na kila wiki wateja saba watapata sh. milioni moja kila mmoja, huku wengine 100 kila wiki watapata muda wa maongezi wa sh. 50,000.

 

 

 

Source: Majira

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents