Burudani

‘Waanze kulana wao kwa wao’ – Mrisho Mpoto

Kama bado haujamkubali Msanii wa nyimbo za asili, Mrisho Mpoto kwa utunzi wake wa Mashairi  na jinsi anavyowasilisha kwenye hadhila basi utakuwa na chuki binafsi ya maendeleo ya sanaa yetu kwani sio kwa hadithi hii ya kufikirika ilivyowakuna watanzania.

Tokeo la picha la mrisho mpoto
Mrisho Mpoto

Mrisho Mpoto ametumia akili ya ziada kuwasilisha ujumbe wake kwa kuelezea mkasa wa Mabaharia waliokuwa na ndoto za kwenda marekani, Safari ambayo ilijawa na dhoruba kibao walivyokuwa njiani na kuwapelekea kuteseka njaa mpaka kulana wao kwa wao,Ipitie hapa hadithi yake ya kusadikika.

Kwa karibia mwezi mzima, mabaharia walikuwa wanajaribu kuvuka bahari ya Atlantic kwenda Marekani ila walikuwa wanazuiwa na mawimbi makali ndani ya bahari hiyo. Meli yao iliharibiwa sana na mawimbi na ikawa haiwezi kutembea tena. Wakabaki katikati ya bahari wasijue cha kufanya. Ilikuwa wazi kwamba wale mabaharia watateseka sana kabla ya kupata msaada wa aina yoyote.

Njaa ilizidi kuwamaliza kwa kasi, wakaamua kuwala paka na mbwa waliokuwemo kwenye meli ile. Njaa iliendelea kuwasakama na wakaamua kula mishumaa yote na kifaa chochote cha ngozi kilichokuwemo kwenye meli yao. Kwa pamoja waliamua sasa waanze kulana wao kwa wao lakini pendekezo hilo lilipingwa vikali na kapteni wa meli ile.

Baada ya wiki mbili, kapteni aliumwa sana na akawa hawezi tena kuwasimamia mabaharia. Waliamua kwa pamoja kucheza mchezo wa bahati nasibu na atakayekosea ndiye atakayeliwa siku hiyo. Baharia mmoja kwa jina Flat alikosea na usiku ule akaliwa. Siku ya pili, mabaharia kwa pamoja waliamua wamle kapteni kwa vile alikuwa mgonjwa sana na ili asiendelee kuteseka waliona ni vizuri wamle. Kapteni alipewa taarifa ya kuliwa kwake na akaanza kusali ili angalau Mungu amuokoe kabla hajaliwa.

Kwenye mida ya saa nne asubuhi, wale mabaharia waliona meli kwa mbali ikija upande wao, waliisubiria kwa hamu huku wengine wakiendelea kunoa visu kwa ajili ya kumchinja kapteni. Kwa miujiza ya maombi ya kapteni, meli ile ilifika kuwaokoa kwenye mida ya saa saba mchana. TWENDE KAZI”.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents