Tia Kitu. Pata Vituuz!

Wanyama amalizana na Tottenham, Mourinho ampa mkono wa kwaheri, amfuata Thierry Henry

Kiungo wa kati wa Tottenham Victor Wanyama amethibitisha kwamba amejiunga na Montreal Impact baada ya Spurs kufikia mkataba na klabu hiyo ya MLS.

Image result for wanyama out tottenham to join thierry henry

Wanyama 28, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Kenya ameiwakilisha Spurs mara nne tu msimu huu.

“Tunamtakia Victor kila la heriu,” klabu hiyo ya Premier League.

Montreal Impact, ambayo mkufunzi wake ni nyota wa zamani wa Arsenal Thierry Henry, iliinyuka New Engand Revolution mabao 2-1 katika mechi ya ufunguzi wa msimu mpya wa MLS siku ya Jumamosi.

Klabu hiyo ya Canada ilimaliza katika nafasi ya tisa msimu wa 2019, baada ya kushindwa kufuzu kwa raundi ya muondoano.

Wanyama alikuwa kiungo muhimu wa Spurs alipotua Southampton Juni 2016, ambapo aliichezea mara 47 katika mashindano yote na kuifanya klabu hiyo chini ya ukufunzi wa Mauricio Pochettino kuibuka ya pili nyuma ya Chelsea katika Ligi kuu ya Premia.

Lakini jaraha la goti alilopata msimu uliofuata, na tatizo la goti lililomuandama msimu wa 2018-19, liliathiri mchezo wake Spurs, hali iliyomlazimu kucheza mechi 24 tu katika mashindano yote.

Spurs ilikubali kumuuza Wanyama kwa euro milioni 13.6 klabu ya Ubelgiji ya Bruges na mwezi Agosti lakini uhamisho huo uligonga mwamba kabla ya muda wa mwishowa uhamisho wa wachezaji.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW