Habari

Babu wa Loliondo aja na utabiri huu

Mchungaji Ambilikile Mwaisapile maarufu kama Babu wa Loliondo, amedai kuwa Mungu amemuonesha utabiri mwingine kwamba, litatokea tetemeko kubwa la ardhi muda wowote na sehemu yoyote duniani, na litadumu kwa masaa manne, lakini halitoweza kuleta madhara yoyote.

Mchungaji Ambilikile Mwaisapile maarufu Babu wa Loliondo

Babu wa Loliondo ameyabainisha hayo wakati akizungumza na EATV, na kusema kuwa licha ya idadi ya watu wanaofika kijijini hapo kupungua kwa ajili ya kunywa kikombe chake, lakini huduma yake bado inaendelea.

“Nimeelezwa na Mungu habari ya tetemeko kubwa, ambalo linakuja na halina madhara, hakuna mtu atakayekufa wala nyumba kuanguka, hata likija usiku mvua inanyesha watu wasikimbie kwenda nje litatikisa masaa manne, kuanzi saa 6:00 na litakata saa 10:00 usiku” amesema Babu wa Loliondo.

Ambilikile Mwasapila maarufu kama Babu wa Loliondo alijipatia umaarufu kwa kutoa dawa kwenye kikombe ambayo wengine walidai kupona magonjwa mbalimbali na wengine hawakupona baada ya kunywa kwenye miaka ya 2011 na 2012.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents