Michezo

Wayne Rooney atakosa mechi muhimu za Man Utd

Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney atakosa mechi ya nyumbani dhidi ya West Ham Jumamosi na pia mechi muhimu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Wolfbsurg kutokana na jeraha.

2EE30E6000000578-0-image-m-26_1449229572661

Rooney mwenye umri wa miaka 30 aliumia kataika mechi waliyotoka sare 1-1 ugenini na Leicester City wikendi iliyopita na atahitajika kusubiri muda zaidi kuchezea klabu hiyo mechi yake ya 500 kutokana na jeraha la kifundo cha mguu.

Louis van Gaal amesema tatizo hilo ni mbaya zaidi ya ilivyodhaniwa, United wanahitajika kushinda mechi ya ugenini dhidi ya Wolfsburg Jumanne kujihakikishia nafasi hatua ya muondoano.

Majeruhi wengine ni Marcos Rojo ambaye ameumia kwenye bega, Phil Jones na Ander Herrera kwa upande mwingine hawataweza kuchezea klabu hiyo dhidi ya West Ham, ingawa Jesse Lingard atarejea.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents