Burudani

Sheddy Clever aelezea furaha yake kukutana na Bizman studio

Mtayarishaji wa muziki wa Burn Records, Sheddy Clever ameelezea furaha yake baada ya kutembelewa na mtayarishaji mkongwe wa muziki, Bizman na kumfunza baadhi ya mambo.

Shebby Clever na Bizman

Sheddy ameiambia Bongo5 kuwa ilikuwa ni ndoto yake ya siku nyingi kukutana na mkongwe huyo aliyekuwa akisikiliza ngoma zake tangu akiwa shuleni.

“Bizman ni mtu ambaye namwelewa sana na namkubali sana toka nipo shule kazi zake nazitambua,” amesema Sheddy. “Kwahiyo nilikuwa nikimtafuta siku nyingi sana lakini nilikuwa simpati kutokana na safari zake lakini kaka yangu Cassim Mganga akaniambia huyu jamaa yupo na ninaweza nikamleta.

Kweli siku ya birthday yangu akanifanyia surprise akamleta hapa, kwa kweli nilifurahi sana. Tukazungumza kuhusu kazi na mambo mengi akanielekeza baadhi ya mambo kama unavyojua huyu ni mkongwe kwahiyo wana vitu fulani adimu sana,” ameongeza.

Bizman ni muimbaji na mcheza kinanda wa In Africa Band na amewahi kushiriki kutengeneza nyimbo nyingi za Bongo Records.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents