Burudani

Makampuni yanapishana kununua vichekesho vya ‘Mkude Simba’ – Kitale

Kitale na Stan Bakora wanaotengeneza vichekesho vya sauti vya ‘Mkude Simba’ wamesema makampuni mengi yamekuwa yakihitaji vichekesho vyao lakini yameshindwa kuvitumia kutokana na kushindwa kufikia makubaliano.

Eid_Tabora-14

Kitale ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa kuna kampuni kubwa ambayo wanajipanga kuingia nayo mkataba.

“Mkude Simba tayari ameshatunufaisha sana, kampuni nyingi zinataka kufanya kazi na sisi lakini wakija wakasikiliza masharti yetu hawarudi tena, yaani kampuni kubwa zote zinapishana mlangoni. Lakini kuna mmoja mkubwa huyo yupo tayari ila wengine ukiwaambia masharti wanakimbia, nahisi wanachukulia poa. Ila sisi tupo vizuri na uongozi wetu upo makini kuhakikisha tunanufaika zaidi na kile tunachokifanya,” amesema Kitale.

Katika hatua nyingine Kitale amewataka mashabiki wa filamu zake kukaa mkao wa kula kusubiri filamu yake itwayo ‘Shobo Dundo’ ambayo pia ndani ya filamu wapo Batuli na Stan Bakora.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents