Michezo

Wayne Rooney kutambulishwa rasmi na DC United 

Mshambuliaji wa klabu ya Everton, Wayne Rooney anatarajiwa kutambulishwa rasmi na  klabu ya DC United inayoshiriki ligi ya Marekani (MLS) leo siku ya Alhamisi.

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, anatarajiwa kuwasili Washington leo na kufanya kikao cha mwisho na klabu hiyo ya Marekani siku ya Jumatatu.

Wayne Rooney kutua Marekani wiki hii kwa vipimo vya afya

Rooney mwenye umri wa miaka 32, anatarajia kuingia kandarasi ya miaka mitatu na nusu ya kuitumikia DC United na kuanza mazoezi na wachezaji wenzake mwishoni mwa wiki.

Hatakama mchezaji huyo anayeongoza kwa magoli kwenye timu ya taifa ya Uingereza atasajiliwa hatotuwa rasmi kwenye kikosi hicho cha DC United hadi hapo dirisha la usajili litakapo funguliwa Julai 10.

Inatarajiwa Rooney mchezo wake wa kwanza atakabiliana na  Vancouver Whitecaps siku ya ufunguzi wa uwanja wa Audi Field jijini Washington.

Mara baada ya kumaliza soka lake kwenye klabu ya Marekani Rooney anatarajiwa kurejea kwenye viunga vya Goodison Park kwaajili ya kuifundisha timu yake ya Everton.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents