Michezo

Wayne Rooney kutua Marekani wiki hii kwa vipimo vya afya

Mshambuliaji wa klabu ya Everton, Wayne Rooney anatarajiwa kuwasili Washington siku ya Alhamisi kwaajili ya mazungumzo pamoja na kufanya vipimo vya afya katika klabu ya DC United inayoshiriki ligi ya Marekani (MLS).

Rooney kutimkia DC United FC ya nchini Marekani

 

Msemaji wa Rooney amethibitisha kuwa nahodha huyo wazamani wa timu ya taifa ya Uingereza atakwenda Marekani na wakala wake, Paul Stretford ili kufanya mazungumzo ya mwisho na Mkurugenzi wa DC United, Jason Levien na Meneja Mkuu, Dave Kasper.

Dili hilo ambalo bado halijakamilika litashuhudia, Rooney akiondoka Goodison Park kwa dau la pauni milioni 12.5 litakalo mfanya kusalia hapo mpaka msimu wa mwaka 2020.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents