Bongo Movie

Wema Sepetu na tetesi za lipstick ya ‘Kiss by Wema’ kupigwa ‘stop’

Meneja mpya wa msanii wa filamu,  Wema Sepetu, amefunguka kuhusu tetesi za bidhaa ya lipstick ya msanii huyo ‘Kiss by Wema’ kuzuiwa kuingia sokoni kutokana na ubora.

Meneja huyo aliyejulikana kwa jina la Happy Shame, amesema mzigo huo haupo sokoni kwa sababu msimu wa kuingiza mzigo mpya bado, na sio kama umezuiwa na serikali kutokana na ubora.

“Hicho kitu sijasikia wala sijatumiwa ’email’ kuambiwa kwamba lipstick zimezuiwa, hivi vitu vinaenda na msimu, muda wake ukifika tutaziachia, kwa hiyo hakuna ukweli isipokuwa kuna baadhi ya vitu tunavikamilisha baadaye mzigo utatoka”, Happy Shame aliiambia EATV.

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kwamba ‘lipstick’ hizo zimezuiwa kuingia nchini kwa sababu hazijakidhi ubora na kwamba ndio sababu ya kutopatikana mtaani kama ambavyo zilikuwa zikigombaniwa, jambo ambalo limepigwa na Meneja wa Wema Sepetu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents