Bongo Movie

Zamaradi afunguka kuhusu vuta nikuvute ya msiba wa Patrick

Mkurugenzi wa vipindi Wasafi TV, Zamaradi Mketema ambaye ndiye aliyepewa jukumu kuratibu msiba wa mtoto wa Muna, Patrick ametaka yeye asihusishwe juu ya mvutano uliopo kati anayedaiwa kuwa ni baba wa mtoto, Mr Peter pamoja na aliyekuwa mke wake Muna Love.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku ya jana kusambaa taarifa mtandaoni kwamba yeye anachangia mgogoro huo kuendelea.

Akiongea na Bongo5 jana anayedaiwa kuwa ni baba wa mtoto Patrick, Peter, alimsifu Zamaradi kwa jitihada zake huku akidai amemwachia jukumu la kuzungumza na Muna ili kuona kama wanaweza kuumaliza mgogoro wao ili mtoto azikwe.

Mapema leo, Zamaradi ameandika ujumbe huu….

NAOMBA NIONGEE

Naona kuna sehemu naingizwa ambazo sidhani kama ninastahili kiukweli (mwenye akili ataona hilo) Huyu mtoto alinigusa sana kwenye ugonjwa wake na ndiomana nikaamua kufanya nilichofanya, na hakuna INFORMATION hata moja niliyoitoa bila kuwasiliana na mwenzetu (Muna) ambae ndie Mama Mzazi kila mtu anafahamu hilo.

Na chochote nilichofanya Nilifanya kwa moyo na roho nyeupe kwa kile ambacho kilionekana na wote kiubinaadamu, since kuna distractions na mambo yamekuwa yana migogoro ya kifamilia, nikiwa kama mtu baki NIMEAMUA KUHESHIMU na kuyaacha KWAO WAO WAYAMALIZE sababu WAO NDIO WANAJUA UKWELI, nitashiriki maziko popote watakapoamua wao (kama watakaa na kukubaliana kifamilia) na sina neno lolote la kutia popote sababu sina ninachojua zaidi na wala sikuwa najua kama kuna kutokuelewana kokote nyuma ya pazia, hivyo tuheshimiane jamani.

Kikubwa tuwaombee maelewano wafikie muafaka na mtoto alale anapostahili, na zaidi MUNGU awaongoze busara iweze kutumika ili Malaika huyu aweze kupumzika kwa amani.

ASANTENI.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents