Burudani

50 Cent atangaza tarehe mpya ya kuachia albam yake iliyoahirishwa toka mwaka 2012

Albam ya rapper Curtis “50 Cent” Jackson III, iitwayo ‘Street King Immortal’ ambayo imekuwa ikiahirishwa kutoka mara kwa mara zaidi ya miaka miwili, sasa inatarajiwa kuingia sokoni baadaye mwaka huu.

50 cent

Mara ya kwanza albam hiyo ilipangwa kutoka November 2012, baadaye ikasogezwa hadi February 2013 na sasa imepewa tena tarehe mpya.

50 Cent, Jumanne wiki hii alipokuwa kwenye red carpet ya uzinduzi wa msimu wa pili wa TV Show yake ya ‘Power’ alitangaza kuwa sasa mashabiki wake wataipata albam hiyo September, 2015.

‘Street King Immortal’ itakuwa ni album ya tano kwa 50 Cent kama solo artist, na ya pili akiwa anajitegemea baada ya kuachana na Interscope Records na Imprint Shady/Aftermath.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents