Inspekta Haroun amjibu Mh. Temba
MWANAMUZIKI mahiri wa kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume Halisi la jijini Dar es Salaam, Haroun Kahena Babu amekamilisha wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Hakuna Mwaka wa Shetani.
na Eugenia Kimolo
MWANAMUZIKI mahiri wa kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume Halisi la jijini Dar es Salaam, Haroun Kahena Babu amekamilisha wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Hakuna Mwaka wa Shetani.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, jijini Dar es Salaam, Kahena ambaye pia ni maarufu kwa jina la Inspekta Haroun, alisema kuwa wimbo huo ni maandalizi ya kukamilisha albamu yake binafsi nje ya kundi itakayojulikana kama Natega Mingo.
Babu alisema kwamba, albamu hiyo itakayokuwa na nyimbo nane, inatarajiwa kuzinduliwa baada ya Sikukuu ya Idd, ambako uzinduzi wake utapambwa na kundi la Wanaume Halisi.
Msanii huyo alizitaja nyimbo zitakazokuwa katika albamu hiyo kuwa ni Binti Kisura, Za Uso aliomshirikisha Issa Shabani Matonya, Ashura, Nianzishe, Haisumbui, Hakuna Mwaka wa Shetani pamoja na Natega Mingo aliomshirikisha Juma Kassim Sir Nature, ambao umebeba albamu.
Babu alisema kuwa, nyimbo za albamu hiyo zimerekodiwa katika studio tatu tofauti, ambazo ni Bongo Records, Up Town Records na Tabasamu Records ya Kenya, ambako amerekodi wimbo Ashura. Alisema kuwa albamu hiyo ipo bomba na amewataka mashabiki kukaa mkao wa kula ili kupata nyimbo zenye ujumbe kwa jamii.