Mtoto Bana al-Abed amshauri Donald Trump kuhusu wakimbizi kuingia Marekani
Baada ya mtoto Bana al-Abed (7) ambaye amekuwa maarufu kutokana na harakati zake za kuwatetea watoto wa nchini kwao Syria pamoja na kumuandikia barua Rais Donald Trump ya kumtaka awasaidie watoto hao, mtoto huyo ametoa ushauri mwingine kwa Rais huyo.
Bana amemshauri Rais Trump atengeneze amani ya nchi nyingine zilizokuwa na vita kwa ajili ya watu wake wasikimbilie nchi nyingine kama anaona kuwazuia kuingia nchini Marekani ni jambo sahihi kwake.
Kupitia mtandao wake wa Twitter, mtoto huyo ameandika, “To @realdonaldtrump: Dear Trump, banning refugees is very bad. Ok, if it’s good, I have an idea for you. Make other countries peaceful.”
Kwa sasa Bana anaishi nchini Uturuki akiwa pamoja na wazazi wake baada ya kufanikiwa kuhamishiwa huko kwa kupata hifadhi mwezi Disemba mwaka jana.