Habari

Polisi wamwachia Freeman Mbowe usiku wa manane

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameachiwa saa saba na robo usiku wa kuamkia leo baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi.

Mbowe alikamatwa Jumatatu hii jioni wakati akienda kujisalimisha polisi na kupekuliwa nyumbani kwake kabla ya kuhojiwa hadi alipoachiwa usiku. Ofisa habari wa chama hicho, Tumaini Makene ameithibitishia Mwananchi Digital taarifa za kuachiwa mwanasiasa huyo kuwa ni za kweli.

Hata hivyo, taarifa iliyosambazwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu kupitia mitandao ya kijamii imesema kuwa chama hicho kitatoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo leo.

“Tunawashukuru wote kwa sala, maombi na subira na hivyo kuhitimisha salama saa kumi za mwenyekiti wetu kuwa chini ya Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam,” Mwalimu amesema.

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents