Serikali kuanzisha mkoa wa Kipolisi Mkuranga
Serikali ina mpango wa kuanzisha mkoa mpya wa Kipolisi wa Rufiji ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kurejesha amani na utulivu katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani.
Kauli hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha bajezi wa Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018
“Kutokana na ongezeko la matukio makubwa ya uhalifu katika wilaya ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji katika mwaka 2107/2018 serikali inatarajia kuanzisha mkoa mpya wa Kipolisi katika maeneo hayo kusogeza huduma ya Kipolisi karibu zaidi na wananchi na kurejesha amani na utulivu katika maeneo hayo,” alisema Mwigulu
Mkoa wa Pwani umekuwa ukikumbwa na matukio ya kihalifu mfululizo ikiwa ni pamoja na Polisi kuuwawa.
Na Emmy Mwaipopo