Habari

Rais Paul Kagame akamata fursa Uingereza, sasa Rwanda kutangaza utalii kwenye jezi za Arsenal

Ukitaja marais barani Afrika ambao wanapenda soka huwezi kumtoa Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye yeye ni shabiki wa kutupwa wa klabu ya Arsenal.

Sasa kutokana na ukaribu uliopo kati ya Rais Kagame na Viongozi wa klabu ya Arsenal huenda ukawa ni chanzo cha nchi hiyo kusaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitangaza nchi Kiutalii.

Kwa mujibu taarifa iliyotolewa na serikali ya Rwanda imeeleza kuwa Jezi za Arsenal kwa miaka mitatu itavaa jezi zenye logo ndogo mkononi zilizoandikwa ‘Visit Rwanda’ kwa lengo la kupromoti utalii.

Logo hiyo itawekwa kwa timu zote za Arsenal za wanaume na wanawake kuanzia msimu mpya wa 2018/19 unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Agosti.

Rwanda kwa mwaka inapokea watalii milioni 1.3 na kwa hatua hii huenda watalii wakaongezeka maradufu ndani ya miaka mitatu.

Urafiki huo pia hautaishia kwenye utalii pekee bali utaenda hadi kwenye uwekezaji kwenye mchezo wa mpira wa miguu nchini Rwanda.

Soma zaidi taarifa iliyotolewa na serikali ya Rwanda – Rwanda unveils three-year partnership with Arsenal to increase tourism, investment and football development .

_______________________________________________________________________________________________

Kwa sasa unaweza kupata habari zetu zote sehemu moja kwa kupitia App yetu ya Bongo5. Pakua sasa kupitia Play Store kwa kubonyeza link hii – https://bit.ly/2J2Argw

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents