Burudani

Wimbo wa Harmonize aliyosema amemshirikisha Diamond Platnumz na Burnaboy wapigwa kalenda, Sallam aingilia kati

Baada ya kutangaza kuwa kuna ujio wa ngoma nne ambazo amewashirikisha wasanii tofauti tofauti ikiwemo ile aliyosema amemshirikisha Boss wake Diamond Platnumz pamoja na msanii kutoka Nigeria Burnaboy, Harmonize alimaarufu Konde boy zimeshindwa kutoka.

Kutokana na sababu ambazo amezitaja ziko nje ya uwezo wake ametangaza zimeshindwa kutoka tarehe 18 ambayo ndio Harmonize alisema zitatoka.

Mbali na hilo Harmonize alimrushia mpira Meneja wa Diamond Sallam Sk na baadaye Sallam kutoa maelezo yafuatayo kuhusu ngoma hizo za Harmonize.

 Maelezo ya Sallam_ Sk “UJIO WA EP YA HARMONIZE @harmonize_tz … Nitatoa maelezo kamili kesho saa nne asubuhi kwanini na imekuwaje haikutoka Tarehe 18 Feb kama ilivyo tangazwa awali, muhimu uwe na bando, maana inafika wakati tusiwadanganye mashabiki zetu kuuficha ukweli ni bora ikae wazi na wao ndio wataamua lipi jema kwao…. Alamsiki tuonane kesho asubuhi saa nne hapa hapa!! #WCB#Wasafi#Harmonize#AfroBongo”

Maelezo ya Sallam ya asubuhi hii ya leo ni haya:-“TAARIFA KWA UMMA.. Maelezo ya utokaji wa EP ya Harmonize @harmonize_tz : Uongozi wa WCB unaomba msamaha kwa ucheleweshaji kama ahadi ya awali ilivyo, muda mwingine msanii anakuwa na shauku kubwa kuwapa mashabiki wake burudani na kufikia sehemu anasahau kuwa hizo burudani pia ni biashara ambayo itakayompatia kipato yeye ili aweze kutoa burudani zingine, kama uongozi lazima tumuandalie misingi ya kibiashara ili anufaike na kazi zake pia, na vilevile tusiwe na matabaka ya kuwajali mashabiki wa sehemu moja pale kazi zinapotoka, inatakiwa kama uongozi kuhakikisha kazi ya msanii inapatikana sehemu zote kukidhi hamu za mashabiki wote, kingine unapofanya kazi na wasanii waliopo lebo kubwa inahitajika lebo zao waweze kutia saini mikataba ya mirabaha ili nyimbo ziweze kuwepo kwenye mitandao yote ya mauzo ili isilete matatizo kwenye lebo zao. Kwahiyo ukubwa wa EP ya Harmonize ilihitaji kupitia yote hayo ili iwe tayari kufika kwa mashabiki, tunashukuru Basata walitoa ushirikiano mzuri kuzikagua nyimbo kwa muda muafaka na hakutokua na tatizo la wimbo unatoka halafu unafungiwa. Kwa haya mafupi sasa EP ya Harmonize ya #AfroBongo itatoka rasmi wiki ijayo chini ya Lebo ya WCB Wasafi. Tunaomba radhi kwa yoyote tuliyemkwaza kwa namna moja ama nyingine tunajua bila nyie mashabiki hakuna WCB. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI BONGO FLAVA 🙏🏽

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents