Habari

Waumini wa kiislam kuanza ibada ya Hijja nchini Saudi Arabia

Zaidi ya waumini milioni mbili wa dini ya kiislam leo siku ya Ijumaa 9 Agosti 2019 wanaanza ibada ya Hijja nchini Saudi Arabia wakati taifa hilo likijaribu kuzuia kutumika kwa ibada hiyo muhimu katika mivutano inayotokota kwenye eneo la Ghuba.

Image result for Hijja Saudi Arabia 2019

Hijja, moja ya mikusanyiko mikubwa kabisa ya kidini duniani, ni kati ya nguzo tano za dini ya kiislam na inapaswa kutekelezwa na kila muumini wa dini hiyo aliye na uwezo walau mara moja katika maisha yake.

Ibada hiyo inajumuisha mfululizo wa shughuli za kidini ambazo hukamilishwa katika kipindi cha siku tano kwenye miji mitakatifu ya dini ya kiislam iliyopo magharibi ya Saudi Arabia.

Ibada ya mwaka huu inafanyika chini ya kiwingu cha mvutano katika eneo la ghuba kufuatia mfululizo wa mashambulizi dhidi ya meli za mafuta, kuangushwa kwa ndege za kijeshi na kuingiliwa kwa shughuli za usafirishaji kwenye mlango bahari wa Hormuz.

Vyombo vya habari nchini Saudi Arabia vimesema kiasi waumini milioni 2.5 kutoka nje ya nchi hiyo watashiriki katika ibada ya mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents