Burudani
Nyimbo tosha ya Pina kuingia sokoni wiki hii
mwanamuziki wa kizazi kipya Karapina anatarajia kuachia sokoni albamu yake ya Nyimbo tosha aliyoizindua mwezi wa 3 mwaka huu, amesema anataraji kuisambaza mwenyewe katika maduka ambayo wamekuwa wakisambaza kazi zao katika siku za karibuni.
Akizungumza na Bongo5, alisema tangu azindue alikuwa bado ajahusambaza mtaani kutokana na sababu ndogo ndogo, hata hivyo amesema atazindua pamoja na Dvd ambayo itaonyesha matukio yote siku ya uzinduzi wa albamu hiyo.
Pia anasema lile tamasha la King Of Stage ambalo mwisho lilifanyika mwaka jana, mwaka huu litafanyika tena, kwa kukutanisha wasanii ambao wataalam wa kulitawala jukwaa. Amesema fomu za tamasha hilo, zitatolewa baada ya kuisha kwa mfungo wa mwenzi mtukufu wa ramadhani mwaka huu.