Burudani

Afande Sele aitaja sababu inayoipoteza hip hop ya Tanzania

Afande Sele amesema mpaka sasa hali inaonyesha kuwa muziki wa Hip Hop hauna nafasi tena nchini.

Afande Sele nzuri_full

Afande ameiambia Bongo5 kuwa waimbaji wengi wa muziki huo wameufanya upoteze mwelekeo.

“Leo hii Singeli au muziki wa kuimba unaonekana unapendwa kuliko Hip Hop,” amesema Afande.

“Unakuta wasanii wetu wengine wanaimba kama 50 Cent, Wiz Khalifa, watu wanashindwa kuimba Hip Hop ya kwetu ya asili, wanaiga Hip Hop ya mamtoni. Kwahiyo wale mashabiki wenyewe wanaona haina haja ya kupenda muziki wa Hip Hop kwa sababu wanachokihitaji hawakipati. Ndio maana unaona muziki wa kuimba sasa hivi unafanya vizuri, lakini muziki wa Hip Hop unapotea kwa sababu pia watu wanaingia kibiashara hawana wito,” amesisitiza.

“Mimi ningeshauri wamiliki wa vyombo vya habari wazungumze na DJs, ndio wanaumaliza muziki wa Hip Hop. Ndio maana sasa hivi Djs wanapiga ngoma kikanda na kuacha kuangalia muziki mzuri.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents