Habari

Afande Sele awachana wanasiasa na waandishi wa habari uchwara wanaohatarisha amani

Msanii mkongwe wa Hip Hop kutoka Morogoro, Afande Sele amesema amani ya Tanzania ipo mikonini mwa Wanasiasa na Waandishi wa habari na kuwataka Watanzania wawe makini kutokana na matukio ya uvunjifu wa amani ambayo yamekuwa yakitokea.

Afande_Sele

Afande amesema kila Mtanzania anawajibu wa kuhakikisha amani iliyopo inaendelea kulindwa na kuepuka Wanasiasa na Waandishi wa habari ambao huchochea na kusababisha matukio ya uvunjifu wa amani.

“Swala la amani, ni haki ya kila mtu na kila mtu ana haki ya kulinda amani kwahiyo tusiyumbishwe na wanasiasa na waandishi wa habari ambao wamekuwa wakiwayumbisha Watanzania,wanasiasa wamekuwa wakiendesha mikutano yao kwa maslahi yao. Kwa mfano swala kodi za “simcard” wamejadili wabunge wetu kwani hawakutambua maisha ya Watanzania? Na Wandishi wa habari wamekuwa wakiandika habari bila uchunguzi wanasababisha machafuko,” ameiambia Bongo5.

Aliendea kusema kuwa suala la ugumu wa maisha linasababishwa na viongozi wetu wanaotambua maisha halisi ya Mtanzania mwenye kipato cha chini.

“Maisha ya watanzania ni magumu,suala la simcard lilijadiliwa bungeni na wakalipitisha wenyewe kwahiyo suala la ugumu wa maisha linasababishwa na viongozi wetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents