Michezo

Aguero apatwa na janga lingine baada ya kunusurika kifo

Ikiwa ni siku tano zimepita tangu mshambuliaji wa klabu ya Manchester City, Sergio Aguero kupata ajali mbaya ya gari nchini Uholanzi iliyompelekea kuvunjika mbavu, mkali huyo wa kucheka na nyavu amepata mshituko mwingine kwa kuachwa na mchumba wake wa miaka minne.

Aguero na Karina

Mchumba wake huyo ajulikanaye kwa jina la Karina Tejeda (31) ambaye pia ni msanii wa muziki nchini Argentina amechukua uamuzi huo akidai kuwa Aguero alikuwa msiri kwenye mahusiano yao.

Mrembo huyo kwenye mahojiano yake na kituo cha runinga cha Telefe cha nchini Hispania amekiri wazi kuwa mawasiliano yake na mshambuliaji huyo yalikuwa ya kusua sua na mara nyingi huwa wanakutana anaporudi kwenye mapumziko ya mechi za kimataifa.

Karina anayefahamika kwa jina la The Princes’ nchini Argentina amesema amekuwa akijihisi mwenye kasoro kwani hata anapoweka posti kwenye mitandao ya kijamii Aguero amekuwa hajibu na hata akimtumia meseji zinachelewa kujibiwa.

Inawezekana sio mzuri, najiona kama si kitu japo tumetoka mbali tumezoeana ila ni vizuri tukaendelea kuishi kwa furaha kama tulivyokutana,“amesema Karina.

Moja ya Tweet zake alizoandika Karina zikimlenga Aguero.

Hata hivyo, mrembo huyo ameongeza kuwa ameshawahi kugombana na Aguero kwa tabia za kwenda klabu na marafiki zake bila kumtaarifu.

Uchumba wa Aguero na Karina uliwavutia Waargentina wengi na ulitajwa kuwa uchumba wenye mvuto nchini humo.

Aguero kabla ya kukutana na Karina alikuwa kwenye mahusiano na mtoto wa mchezaji wa mpira wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina, Diego Maradona, Giannina Maradona  na walifanikiwa kupata mtoto mmoja.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents