Burudani

Albamu ya Chin Bees ‘Ladha’ kutolewa bure (+video)

Baada ya kuachia albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Ladha, msanii wa muziki Bongo, Chin Bess ameweka wazi kuwa albamu hiyo itapatikana bure kabisa kwa njia zote zile.

Chin Bees amesema sababu ya kufanya hivyo ni kwamba mwaka jana mashabiki wake walifanikisha ngoma yake ya Kababaye kufika mbali, hivyo albamu hiyo ni zawadi kwao.

“Kwa hiyo hii ni kama zawadi kwa mashabiki wangu, nimewaletea hii wafurahi inapatikana bure kabisa, unaweza ku-downlod mtandaoni ni bure kabisa, hivyo narudisha upendo kwao,” amesema.

Chin Bees ni msanii wa kwanza wa Bongo Flava kutoka albamu kwa mwaka huu mara baada ya Vanessa Mdee kufanya hivyo mwishoni mwa mwaka jana. Pia mwaka huu wasanii kama Wakazi na Diamond wanatarajiwa kutoa albamu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents