Michezo

Mashabiki wa Arsenal waombwa radhi baada ya kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Brighton

Mashabiki wa klabu ya Arsenal wameombwa radhi na mlinda mlango wa klabu hiyo, Petr Cech kufuatia kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion.

Petr Cech

Petr Cech (35) kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa ni mbaya ukiwa kama mlinda mlango wa timu inayoshiriki ligi bora duniani kama EPL na kuruhusu kufungwa magoli mawili na kuwataka mashabiki na wadau wa klabu ya Arsenal kukubali matokeo.

Kama unataka kushinda mchezo wa ugenini katika ligi bora duniani, Mlinda mlango huwezi kuruhusu magoli mawili kama nilivyo fanya mimi leo. Kwa kweli hilo haliwezekani, tumejitahidi kurudisha ili tushinde mchezo huo lakini imeshindikana,“amesema Petr Cech.

Soma na hii – Arsenal yageuzwa kitoweo EPL, Yapokea kipigo kingine mashabiki wasema ‘Wenger Out’

Hata hivyo, mashabiki wa Arsenal kwenye mchezo wa jana uwanjani walibeba mabango yaliyoandikwa ‘Wenger Out’ wakishinikiza kocha wa klabu hiyo aachie ngazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents