Habari

Alichozungumza aliyekuwa mke wa Bilionea Msuya, mwenzake mara baada ya kuachiwa huru

Jana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilimuachia huru aliyekuwa mke wa mfanyabiashara maarufu wa madini jijini Arusha, Erasto Msuya maarufu Bilionea Msuya, Miriam Mrita na mwenzake Revocatus Muyella baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.

Hata hivyo wawili hao mara baada ya kuachiwa huru kwa mara ya kwanza walifunguka mbele ya waandishi wa habari na kuonyesha furaha yao baada ya kuachiwa huru.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mrita alisikika akisema “Namshukuru Mungu, utukufu kwa Mungu, utukufu kwa baba, Yesu ni mwema,” amesema

Naye Muyella akizungumza na waandishi wa habari alisema kitu ambacho amekimisi uraiyani ni watoto wake.

“Siwezi kuongea bali tunamshukuru Mungu, mapambano kwa kweli yalikuwa makubwa, kitu ambacho nimekimis uraiyani ni watoto wangu,” amesema Muyella

Washtakiwa hao wawili walikuwa wakikabiliwa na shtaka moja la mauaji ya kukusudia la kumuua Anetha Msuya ambaye alikuwa mdogo wa Bilionea Msuya.

Aneth aliuawa kwa kuchinjwa na kitu chenye ncha kali nyumbani kwake Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam Mei 25, 2016.

Akitoa hukumu hiyo Jaji Edwin Kakolaki amesema kuwa baada ya kujiridhisha pasipo kuacha shaka, mahakama inawaachia huru wawili hao kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents