Burudani

Alikiba afungua milango nchini Rwanda, Haruna Niyonzima ahusishwa

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba ni moja ya wasanii ambao wanakubalika sana nchini Rwanda tangu miaka hiyo, hii bila shaka yoyote ni kutokana na ubora wa kazi zake, ambapo amekuwa akiwavutia wapenzi wengi wa muziki nchini humo.

Bahati na Alikiba

Kufuatia kukubalika nchini humo Alikiba tayari ameshakubali kufanya kazi na Msanii maarufu nchini Rwanda, Bahati kutoka katika kundi la Just Family.

Akithibitisha taarifa hizo, Bahati amesema alipata tabu kutafuta namba za simu ya Alikiba mpaka alipopewa na mchezaji wa Klabu ya Simba, Mnyarwanda Haruna Niyonzima.

“Tulipitia njia nyingi tukapata namba yake tukaonana ana kwa ana hapa Rwanda, tumeunganishwa naye na Haruna Niyonzima maana Haruna ni rafiki yake na Alikiba tena ni rafiki yetu pia,” amesema Bahati kwenye mahojiano yake na mtandao wa Habari Pevu wa nchini Rwanda.

Akifafanua kuhusu kolabo yake na Alikiba, Bahati amesema “Alikiba ni msanii ambaye namkubali sana tena tuna deal na yeye. Alikiba ni mheshimiwa tunamheshimu, ndani ya Dar es Salaam kuna wasanii wengi tena wote ni masupastaa, kuna huyu Harmonize, kuna Diamond, Rayvanny, Richi Mavoko, lakini tunayetaka kufanya kolabo na Alikiba,”.

Hata hivyo, tayari Alikiba ameshamfungulia milango msanii huyo kwa kumkubalia ombi lake mwezi Januari mwaka huu wakati alipoenda Rwanda kwenye tamasha la East African Party.

Tukipata muda tunakwenda kumuona Dar es Salaam, yaani anatusubiri sisi ndo tunaangalia muda wetu. Ameshatukubalia collabo, yuko tayari tena sana,“amesema Bahati.

Kwa upande mwingine, Bahati amesema kuwa kwa muda huu hawezi kuja Dar es Salaam kukamilisha kolabo hiyo kutokana na maandalizi ya tamasha ya Guma Guma.

Soma na hii – Alikiba aitikisa Kigali, Ajaza uwanja wa mpira (Picha+Video)

Tamasha la Guma Guma au maarufu kama Primus Guma Guma Superstar ni moja ya matamasha makubwa ya kutafuta vipaji nchini Rwanda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents