Ancelotti aanza na Bale ndani ya Madrid

Kocha mpya wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema kuwa yupo tayari kumrudisha aliyekuwa mchezaji wa klabu hiyo Gareth Bale.

Katika mazungumzo yake hapo jana baada ya kutambulishwa rasmi, Ancelotti amedai anatarajia Bale atarudi na atafanya vizuri akitoka Tottenham ambapo anacheza kwa mkopo.

”Gareth hajacheza sana Premier League, lakini amefunga magoli, namfaha vizuri tu kama akihamasika anaweza kuwa kwenye msimu mzuri”- amesema Ancelotti.

Ancelotti amemtaja Bale zaidi ya mara tatu wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari akiwa kama kocha mpya wa Real Madrid kwa kusaini kandarasi ya miaka mitatu.

Kocha ameongeza kuwa anatarajia wachezaji kama Bale na wengine kama vile Isco na Marcelo ambao wamepoteza nafasi zao chini ya Zidane watafanya mazoezi kwa bidii ili kumuonyesha kocha wao kuwa wanania ya kuichezea Real Madrid.

Bale alionyesha kiwango kikubwa sana chini Ancelotti msimu wa mwaka 2013-14, akifunga magoli kwenye mchezo wa fainali wa Champions League na Copa del Rey na kumsaidia kutwaa mataji hayo ndani ya Real Madrid.

Related Articles

Back to top button