Bongo Movie

Antu Mandoza wa Kiumeni: Bado niko single

Mwanadada Antu Mandoza ‘Miss Mandoza’ ambaye alionyesha uwezo mkubwa katika filamu ya ‘Kiumeni’, amedai bado yupo sigle ambapo kwa sasa anatafuta mtu sahihi ambaye anaweza kuingia naye kwenye maisha ya ndoa.

Muigizaji huyo anaomba kila siku Mungu amjalie apate mwenza ambaye atajali na kuithamini kazi yake, ili kukwepa changamoto wanayokutana wasanii wenzake wa kike kuzuiwa kufanya kazi zao.

“Nasali kila siku Mungu anipe utashi kupata mtu atakayekua mume na mwenza wangu ambaye hataiona kazi yangu kuwa ni kikwazo, bali anipe sapoti ya kutosha kuendeleza kipaji changu,” alisema Antu.

Antu aliyewahi kushiriki tangazo la shindano ya Bongo Star Search ‘Fungua Njia’ 2011 lililotengenezwa India, aliwashinda wenzake kama utani kutokana na kipaji kikubwa alichonacho katika uigizaji na kujiamini kwake mbele ya kamera.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents