Michezo

Argentina ya mtimua kocha wao Edgardo Bauza

Kocha Edgardo Bauza hatimaye ametimuliwa katika timu ya Taifa ya Argentina kutokana na chama cha soka nchini humo kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.

Muargentina huyo amefukuzwa akiwa ameiongoza timu hiyo kwa mechi 8 tu na kuiacha katika wakati mgumu kwenye mbio za kufuzu michuano ya kombe la Dunia 2018 Russia.

Argentina ambayo inaongozwa na nahodha Lionel Messi ambaye amefungiwa na FIFA mechi 4 , ipo katika nafasi ya 5 kwenye kundi la Amerika kusini la kufuzu kombe la dunia huku zikiwa zimebaki mechi 4.

Timu 4 za juu zitafuzu moja kwa moja kombe la dunia wakati timu ya 5 itacheza mtoano na timu kutoka Oceania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents