Burudani

Ariana Grande na Big Sean waachana!

Baada ya kukaa kwenye uhusiano kwa miezi nane, mastaa wa muziki nchini Marekani, Ariana Grande na Big Sean wameachana.

big-sean-ariana-grande

Wapenzi hao wametangaza kuachana kwao kwa maelezo ya pamoja kupitia wawakilishi wao. “Wote bado wanajaliana na wanabaki kuwa marafiki wa karibu. Tunaomba vyombo vya habari kuheshimu faragha yao kuhusiana na suala hili binafsi kwa sasa,” yalisema maelezo.

Ariana, 21, na Sean, 27, walianzisha kuwa na uhusiano August 2014.

Kwa mujibu wa Us Weekly, wawili hao waliamua kuachana kimya kimya wiki chache zilizopita.

“Waliamua kuchukua uamuzi wa kuachana kwasababu ya kutofautiana kwa ratiba za ziara zao ambazo zingewafanya wawe mbali mwaka ujao,” kilisema chanzo cha karibu yao.

Kabla ya hapo Sean, alikuwa amemchumbia Naya Rivera.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents