Habari

Auawa na kutenganishwa kichwa na kiwiliwili

Mkazi wa Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana na kichwa chake kukitenganisha na kiwiliwili.

Na Juddy Ngonyani, Sumbawanga



Mkazi wa Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana na kichwa chake kukitenganisha na kiwiliwili.


Marehemu huyo ni Modest Nkondo (60), mkazi wa kitongoji cha Tululu, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Bw. Germanus Mponguliana, alisema tukio hilo la kinyama lilitokea Novemba 26, mwaka huu nyumbani kwa marehemu huyo.


Kamanda Mponguliana alisema watu wasiojulikana, waliivamia nyumba ya marehemu huyo na kuvunja mlango, kuingia ndani kumcharanga kwa mapanga baadaye kumchinja na kutenganisha kichwa na kiwiliwili.


Alisema kabla ya mauaji hayo, saa 12:00 jioni, ndama wawili wa marehemu huyo walijeruhiwa kwa mapanga na Khatibu Chakari (25), mkazi wa kitongoji hicho baada ya kudaiwa kuharibu mazao yake.


Kamanda Mponguliana alisema polisi inamshikilia Chakari kwa uchunguzi.


Aidha, alisema upelelezi zaidi kuhusiana na mauaji hayo unaendelea kubaini wauaji hao na chanzo chake.


Hata hivyo, alisema upelelezi wa awali unahusisha mauaji hayo na imani za kishirikina.


Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents