Burudani

AY asema yuko tayari kuwasaidia wasanii wa Tanzania wanaotaka kupata connection za kimataifa

Miongoni mwa vikwazo vinavyochangia wasanii wa Tanzania wanaofanya vizuri kimataifa kuwa wachache, ni pamoja na wengi wao kukosa connection na hivyo kushindwa kujitangaza kimataifa.

AY

Ambwene Yessaya a.k.a AY ambaye ameanza kutengeneza connection zake miaka mingi iliyopita, amesema yuko tayari kuwasaidia wasanii wengine watakaohitaji msaada wake kuwaonesha njia za kupita kufikisha kazi zao na kujitangaza kimataifa.

“Kwanza jambo la kwanza ambalo nataka kuwaambia watu ni kuwa nikifanya hizi kazi sifanyi kazi kwaajili yangu peke yangu…uliza mtu yoyote ambaye ametoboa ameweza kwenda nje, kwa njia moja ama nyingine lazima alipita kwangu kupata connection, kutambulishwa sehemu na vitu kama hivyo.” Alisema AY kupitia The Jump Off ya Times Fm.

“Kwahiyo navyopata connection zangu ni kwaajili ya watu wote, na ninawaambia hata watu wengine kwamba mkihitaji kama ni msaada wa kujuana na watu na vitu kama hivyo mimi nipo nafanya kazi kwa ajili ya watu wote.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents