Burudani

AY awachukua Hermy B na Marco Chali kwenye mradi mpya

AY amewachukua Hermy B na Marco Chali kutengeneza ngoma yake mpya.

11252465_1647628742120195_616091842_n
AY akiwa studio na producer wa B’Hits, Hermy B na producer wa MJ Records, Marco Chali

AY ameshare picha hiyo juu akiwa studio na watayarishaji hao wakubwa nchini wanaowakilisha studio maarufu zaidi, Hermy B wa B’Hits na Marco Chali wa MJ Records.

Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza AY anakutana tena studio na Hermy B baada ya kuwahi kupishana katika masuala ya kibiashara mwaka 2012.Baada ya hapo AY amekuwa akifanya kazi zaidi na Marco.

“Unategemea kitu kitatokaje?? Best Producers @marcochalitz & @hermyb kwenye chumba kimoja na Mzee wa Commercial.. BIT TINGZ R GWAN!! #ZEE #ElCapo #FAYAAAA #KofiazaMarcoChali,” ameandika AY.

Mashabiki wameonesha kufurahishwa mno na picha hiyo na matarajio yao ni makubwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents