Technology

Baada ya Facebook kuinunua: Whatsapp yapotea hewani kwa zaidi ya saa 3, watumiaji wakasirika

Jumamosi hii WhatsApp ilipotea hewani kwa zaidi ya saa tatu na kuwakera watumiaji wengi ikiwa ni siku chache baada ya Facebook kutangaza kuinunua kwa dola bilioni 19.

whatsapp

“Huduma ya WhatsApp imerejea tena. Tunaomba radhi kwa kutopatikana,” WhatsApp iliomba radhi kupitia Twitter jana. Mapema iliandika kuwa huduma hiyo ilikuwa imekumbwa na tatizo la server bila kutoa maelezo zaidi.

WhatsApp iliyoanza miaka mitano iliyopita ina jumla ya watumiaji milioni 450 duniani na kila siku watu milioni 1 huongezeka.

Baada ya huduma hiyo kukata, watumiaji wake walitumia mitandao mingine kama Twitter kutoa malalamiko yao huku wengine wakianzisha topic kwenye Twitter iliyopewa jina #Whatsappdown.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents