Burudani

Baba Levo ataja maendeleo aliyoyapeleka kwenye kata ya Mwanga

Baba Levo ambaye ni diwani wa Mwanga Kaskazini mkoani Kigoma amefunguka maendeleo yake katika uongozi huo katika kipindi cha mwaka mmoja tangu alipochaguliwa kukalia kiti hicho.

Akiongea katika kipindi cha Mega Mix cha Abood FM ya Morogoro, Baba Levo amesema katika kipindi alichokaa katika uongozi huo tayari amewasaidia wananchi wake kwenya Afya, elimu na miundombinu kwa asilimia kubwa.

“Cha kwanza kabisa ni kufufua zahanati ambayo ilikuwa imekufa inawapa mateso zaidi wananchi wa Mwanga Kaskazini wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kupata huduma za kiafya wakati kuna zahanati katika kata yao. Kwahiyo nimeifufua na kuifanya iweze kutoa huduma kama kawaida,” amesema.

“Kwa upande wa elimu nimeweza kumaliza matatizo hayo katika shule zangu. Mimi nina shule tano katika kata yangu, kwahiyo shule tatu nimefuta tatizo la madawati zimebakia katika shule mbili ambapo nina nuhakika katika kumaliza mwaka huu na kwenyewe nitakuwa nimefuta tatizo la madawati. Na pia nimeweza kupigania kupata walimu wa Sayansi katika kata yangu, walimu wa sayansi wamekuwa tatizo kubwa siyo katika kata yangu tu bali ni Tanzania nzima. Nimepambana nimeweza kupata walimu takribani wanne wa sayansi,” ameongeza.

“Niliwaahidi wananchi wangu kuwajengea soko la jioni ambalo watakuwa wanafanya shughuli zao kwa uhuru bila kubuguziwa kwa kuwa kutakuwa na mwanga ambao utatokana na taa za sola zenye thamani ya shilingi milioni 35. Nashukuru mpaka sasa tumeshakamilisha kuweka taa imebakia tu kusakafia chini ili mambo yaweze kwenda.”

Wakati huo huo kiongozi huyo amesisitiza kuwa kata yake ina matatizo makubwa ya barabara, lakini tayari amepata barabara nne ambazo zinapita katika mitaa ambayo ilikuwa haipitiki hapo mwanzoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents