Michezo

Baba mzazi wa Eden Hazard asuka mipango kabambe mwanae kutimkia Real Madrid

Baba wa nyota wa Chelsea, Eden Hazard ambaye ni Thierry ameripotiwa kufanya mazungumzo na klabu ya Real Madrid siku chache kabla ya mchezo wa fainali wa klabu bingwa barani Ulaya ili kuona kama mwanaye anaweza kujiunga na miamba hiyo ya Hispania.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Hazard ameitumikia klabu ya Chelsea kwa miaka sita sasa na kufanikiwa kutwaa makombe mawili ya ligi kuu nchini Uingereza na moja la Europa League akiwa hapo Stamford Bridge.

Aliyekuwa meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane alikuwa kwa miaka mingi akitamani uwezo wa Hazard licha ya kuwa hayupo ndani ya timu hiyo kwa sasa ila bado amekuwa akitakiwa na miamba hiyo ya La Liga.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Marca, Mzee Thierry amelichukulia jambo hilo kwenye mikono yake mwenye mpaka kuhakikisha linatimia na Real Madrid kumsaini kijana huyo mwenye umri wa miaka 27.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents