Burudani

Babu Tale: Dogo Janja aseme ukweli wa kilichotokea, tutamsamehe

Boss wa Tip Top Connection, Babu Tale amesema yeye amemsamehe Dogo Janja na hana tatizo naye ila amemtaka asema ukweli wa kilichotokea.

page

“Aongee ukweli tu haina shida, nimemsamehe yeye ni Muislamu mwenzangu tumetumwa tusameheane, mimi nimeshamsamehe ila nimezungukwa na mashabiki ambao wakati yeye ananitukana kuna mashabiki ambao walikuwa upande wangu ingawa walikuwa hawajui kama dogo alikuwa anaongea ukweli au uongo,” Tale ameiambia tovuti ya Times FM.

“Dogo anatakiwa aseme kama kweli aliibiwa, kama kweli alidhurumiwa na kama kweli hajawahi kuishi nyumbani kwa Madee. Anatakiwa aongee dhahiri asifiche, aongee tu ukweli,” ameongeza.

“Siku zote kwenye ukweli uongo hujitenga, wakati yuko South Africa alipost picha ‘ningekuwa Tip Top nisingefika huku’. Nilishangaa heeh huyu kutoka huko kijijini kwao alifanyaje hadi kufika hapa. Wazazi wake nao wakawa wamekubali uongo wa mtoto wao wakaanza kutuongelea na sisi maneno ambayo ni uongo. Ulikuwa uongo wa watoto halafu bado wao wanakandamiza uongo zaidi ya uongo. Kwa kuwa ni mtoto kuna wazazi ambao walisimama nyuma yake ambao nao walikuwa wanasapoti. Aongee ukweli mimi ntamsaidia.”

Source:Tovuti ya Times Fm

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents