HabariMichezo

Baerbock apigilia msumari: Maoni ya Rais Macron ni ya Ulaya

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema Ulaya inao mtazamo sawa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, juu ya uhusiano baina ya Ulaya na China.

Baerbock ametoa kauli hiyo baada ya Rais Macron kusema Ulaya inapaswa kuwa na sera yake juu ya China na Taiwan badala ya kuifuata tu Marekani.

Matamshi hayo ya Rais wa Ufaransa yalikabiliwa na mashambulizi makali kutoka Marekani na washirika ndani ya Ulaya.

Akijibu ukosoaji huo dhidi ya Rais Macron, Baerbock amesema anataka kusisitiza kuwa sera ya Ufaransa kuhusu China ni taswira sahihi ya sera ya Ulaya.

Akiwa mjini Tianjin, Waziri Annalena Baerbock ameunga mkono kauli hiyo ya rais Macron iliyosababisha utata na kuongeza kuwa ”Nguvu ya Umoja wa Ulaya haitokani tu na kuwa nchi wanachama ziko karibu, lakini pia zinatokana na ukweli kuwa zinafuata mkakati mmoja kuhusu masuala ya msingi kwa maslahi na maadili yao.”

Vile vile ameonya dhidi ya kupanuka kwa mzozo wa Taiwan.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents