Burudani

BAJETI 2017/18: Tuwaombee walevi na wavutaji wasigome – Afande

Msanii wa muziki wa hip hop, Afande Sele ameipongeza bajeti mpya ya serikali ya mwaka 2017/18 huku akidai kwa sasa Taifa lina kila sababu ya kuendelea kuwaombea watu wanaovuta sigara na walevi wa pombe kwa kuwa kila mwaka ndiyo watu ambao wanaibuka vinara kwenye kuchangia kulijenga taifa kwa mapato.

Afande Sele amesema hayo baada ya wiki hii Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kuwasilisha bungeni mapendekezo ya makadirio ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2017/18 ambapo Afande Sele anakiri kuwa ni kweli bajeti hiyo ni nzuri na kusema kama Taifa halijawahi kuwa na bajeti mbaya sana bali huwa na tatizo kubwa katika utekelezaji wa mipango hiyo.

“Kweli bajeti ya mwaka huu ni nzuri sana kabisa. Ingawa kama Taifa hatujawahi kuwa na bajeti mbaya sana,” Afande Selle aliiambia EATV.

“Lakini tumewahi kuwa na utekelezaji mbaya sana wa malengo ya bajeti miaka yote. Mipango siyo matumizi haya basi tuendelee kuwaheshimu na kuwaombea walevi na wavutaji wasigome, wasiugue na ikibidi wasife mapema ili waendelee kuwa vinara wa kulichangia na kulijenga Taifa kupitia ongezeko la kodi kwa bidhaa zao kila mwaka,” aliongeza Afande Sele.

Afande Sele alisema haya baada ya serikali kuendelea kupandisha kiwango cha ushuru kwenye vinywaji baridi, bia pamoja na sigara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents