Habari

Baraza la kijiji laamuru dada wa kaka aliyebaka abakwe (+Video)

Jeshi la polisi nchini Pakistan linawatafuta wajumbe 20 wa Baraza la kijiji cha Raja Ram katika mji wa Muzaffarabad nchini humo ambao walitoa amri ya kubakwa kwa dada wa kaka aliyembaka msichana wa miaka 12 ili kulipiza kisasi kwenye familia hiyo.

Mtoto aliyebakwa akiwa na mama yake kwenye mahojiano waliyofanya na Gazeti la DAWN la nchini humo .

Baraza la kijiji hicho liliamuru msichana huyo (dada wa mbakaji) mwenye miaka 16 abakwe wiki alhamisi ya wiki iliyopita ili kulipiza kisasi cha unyama uliofanywa na kaka yake jumatatu ya wiki iliyopita.

Msichana huyo alikamatwa na kubakwa na vijana watano walioteuliwa na Baraza hilo mbele ya wazazi wake kwa lengo la wazazi kuona uchungu kama wazazi wa mtoto aliyebakwa na kijana wao.

Eneo la tukio ambalo wazee wa Baraza na wazazi walishuhudia mtoto wao akifanyiwa ukatili huo kwa amri ya Baraza.

“Baada ya kupata taarifa kuwa kijana wetu amebaka tulienda kuomba msamaha lakini wakasema ili waweze kutusamehe ni lazima twende na dada wa Amrih (Mbakaji) tukafa hivyo kisha wakatupeleka kwenye baraza la kijiji na kuamuru msichana wetu nae abakwe mbele ya yetu ili kulipiza”,amesema Muhammad Bilal kaka wa Mbakaji kwenye mahojiano yake na Gazeti la DAWN .

Chumba cha Mbakaji

Baraza hilo linalotambulika kwa jina la Jirgas linaundwa na wazee 40 ambao kazi yao kubwa ni kutatua kesi mbalimbali za kijiji hicho ingawaje .

Kamada wa Polisi wa mji wa Multan , Saliim Khan Niyazi amesema mkuu wa baraza hilo lililotoa hukumu ya kubakwa na wajumbe wengine 20 wametiwa nguvuni na kwamba mtuhumu mkuu ametoroka na anatafutwa na vyombo vya dola.

Hata hivyo, Mkuu wa jimbo la Punjab, Shahbaz Sharif ameliamuru jeshi la polisi kuwasaka na kuwakamata wajumbe wote wa baraza la kijiji hicho ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Matukio kama hayo sio mageni nchini Pakistan kwani kama hilo la maamuzi ya mabaraza ya vijiji lilitokea mwaka 2002 ambapo mwanamke mmoja ajulikanae kwa jina la Mukhtar Mai aliamriwa kubakwa na kundi la vijana ingawaje alienda kutoa taarifa Polisi na kitendo hicho cha kishujaa kimemfanya awe maarufu zaidi duniani.

Mabaraza ya vijiji yanatambuliwa kuwa ni mbadala wa mahakama dhaifu nchini Pakistan ambazo huchelewesha kesi zinazowasilishwa kwa miaka mingi na maamuzi ya mabaraza hayo yanakubaliwa na wakazi wa maeneo ya vijiji hivyo, ingawa hayatambuliwi rasmi na serikali ya Pakistan.

 

By Godfrey Mgallah

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents