Burudani

Belle 9 ajutia mtindo wake wa kukaa muda mrefu bila kutoa ngoma

Belle 9 amegundua kuwa kukaa kwake kimya muda mrefu bila kutoa ngoma, kulikuwa kukiwakera mashabiki wake.

Belle9

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa sasa hivi amejipanga kuachia ngoma baada ya ngoma ili kuwapa mashabiki wake kitu wanachotaka!

“Baada ya video ya Vitamin Music, mashabiki wa muziki wangu wameonyesha kuchoshwa na ukimya wangu, wanasema ‘mbona unakaa kimya sana bila kutoa ngoma! Yaani kukaa muda mrefu bila kutoa ngoma wakati wasanii wengine wanatoa mpaka ngoma sita wanajisikia vibaya,” amesema.

“Sasa nimegundua mashabiki wanakuwa disappointed ndio maana licha ya kuachia video ya Vitamin Music, nimeachia ‘Shauri Zao’ ili kukata kiu zaidi kwa mashabiki wangu ambao wamechoshwa na ukimya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents